Baada ya bomoabomoa dar ona majibu yaliyotolewa mahakamani kisutu

list-style: none; margin-bottom: -1px; outline: none; padding: 0px; text-align: center;">
Wakazi  wanaodaiwa kubomolewa nyumba zao za mabondeni wakiwa wamekaa nje ya Maduka yaliyopo karibu na eneo la mahakama hiyo.
KESI ya kupinga bomoabomoa iliyofunguliwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi jijini Dar es salaam imeunguruma tena leo ambapo baadhi ya wakazi waliobomolewa nyumba walionekana kukusanyika nje ya mahakama hiyo.
Kesi hiyo namba 822 ya mwaka 2015 inasikilizwa na Jaji Penterine  Kente huku upande wa walalamikaji wakisimamiwa na wakili Abubakar Salim.
Kamera yetu ya mtandao huu wa Gpl ilifika mahakamani hapo leo asubuhi  na kukuta wananchi hao wakiwa nje ya mahakama hiyo na ilikuwa bado haijaanza kusikilizwa muda wa saa tano asubuhi. Wananchi hao walijikusanya nje kama picha zinavyoonesha.
Share on Google Plus
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.