Kilimanjaro Music Tour yabisha hodi Moshi


Ziara ya Kilimanjaro Music Tour ambayo ndio gumzo kubwa sasa katika sekta ya 
burudani imebisha hodi katika Mji wa Moshi ambapo wapenzi wa muziki wanatarajiwa 
kupata burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali Jumamosi hii.
Maandalizi yote yamekamilika huku zaidi ya wasanii 10 wa humu nchini wakitarajiwa 
kutua mjini hapo Ijumaa tayari kwa show kubwa itakayofanyika katika Viwanja vya Chuo 
Shirikishi cha Ushirika na Biashara (MUCCOBs).
Ziara hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanajro Premium Lager ambayo imekuwa mstari 
wa mbele katika kufikisha muziki wa Tanzania kwenye kilele cha mafanikio. Ziara hii 
inaratibiwa na EATV na East Africa Radio, Executive Solutions, Integrated na AIM.
Wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Ommy Dimpoz, Kala Jeremiah, Weusi, Ben 
Pol, Jambo Squad, Young Killer, Ney wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Warriors na 
Professor J.
“Wasanii wote wako tayari kutoa burudani ya aina yake na sisi kama wadhamini 
tunawaahidi wakazi wa Moshi mambo mazuri...waje kwa wingi wakutane na wasanii 
wao na pia wapate burudani bila kusahau Bia yao namba moja Kilimanjaro Premium 
Lager,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.
Alisema kiingilio katika show hii itakayoanza saa nne asubuhi ni Tsh 2500 na kila 
atakayeingia atapewa bia ya bure mradi ametimiza umri wa miaka 18 na show itaanza 
saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
Tiketi wa ajili ya show hii zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa pale MUCCOBs na pia 
promosheni mbalimbali za kusisimua zinaendelea katika baa tofauti Mjini Moshi.
“Ziara hii sio ya washindi wa Tuzo za Muziki (Kilimanjaro Music Awards) bali ni ziara ya 
wasanii ili waweze kutangaza kazi zao pamoja na kupeleka burudani mikoani ili watu 
wanaokaa huko pia waweze kufaidi,” alisema Bw Kavishe.
Aliongeza kuwa wasanii wana nafasi kubwa sana kueneza ujumbe mbalimbali katika 
jamii hivyo wanapaswa kuungwa mkono ili waweze kuwafikia wananchi wakiwemo wa 
mikoani.
Ziara hii itahusisha mikoa ya Moshi, Mwanza, Kigoma, Kahama, Iringa, Mbeya, 
Dodoma, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam na inaanzia Mkoani Moshi Mei 24, Mwanza 
Mei 31, Kahama Juni 7, Kigoma Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9, Dodoma 
Agosti 16, Tanga Agosti 23, Mtwara Agosti 30, Dar es Salaam Septemba 6,” alisema 
Kavishe.
Share on Google Plus
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.